Swali: Jina ´Abdun-Nuur ni katika majina ya vinavyoabudiwa badala ya Allaah?
Jibu: Halikuthibiti hili. Katika Majina Yake ni An-Nuur (Subhaanahu wa Ta´ala) na hili halina shaka. An-Nuur ni katika Majina Yake na vilevile Nuur ni katika Sifa Zake (Jalla wa ´Alaa). Lakini hakukuthibiti kwamba mtu anasibishe uabudiwa na Nuur. Kufanya hivi kuna kujifananisha na dini ya wafursi ambao wanaabudu nuru na giza.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-5-11.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014