Swali: Jina ´Abdun-Nuur ni katika majina ya vinavyoabudiwa badala ya Allaah?

Jibu: Halikuthibiti hili. Katika majina Yake ni an-Nuur (Subhaanahu wa Ta´ala) na hili halina shaka. an-Nuur ni katika majina Yake na vilevile an-Nuur ni katika sifa Zake (Jalla wa ´Alaa). Lakini hakukuthibiti kwamba mtu anasibishe uabudiwa na an-Nuur. Kufanya hivi kuna kujifananisha na dini ya wafursi ambao wanaabudia nuru na giza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-11.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014