Swali: Je, Ibn Siynaa na ar-Raaziy ni wakanamungu? Tumesoma masomoni ya kwamba ni wanachuoni na matabibu ambao ni waislamu.

Jibu: ar-Raaziy sio kama Ibn Siynaa. ar-Raaziy ni Ash´ariy. Ni kweli kwamba alikuwa ni Ash´ariy. Lakini alikuwa ni mwanachuoni ambaye alikuwa na msimamo na ukati na kati. Inasemekana kuwa mwishoni mwa uhai wake alitubia. Tofauti na Ibn Siynaa ambaye ni mkanamungu. Asilinganishwe huyu na huyu. Isitoshe ar-Raaziy hakuwa Suufiyyah. Alikuwa ni katika wanachuoni wa falsafa na wanachuoni wa mantiki. Madhehebu yake yalikuwa Ash´ariyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (14) http://alfawzan.af.org.sa/node/2057
  • Imechapishwa: 16/04/2017