al-Fawzaan Kuhusu Funga Na Ftari Za Pamoja Zimezozushwa Na Vijana


Swali: Wito wa watu kufunga kwa pamoja na kufuturu kwa pamoja unajuzu? Ni jambo limefanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapana. Hii ni Bid´ah. Hii ni Bid´ah. Kufuturu kwa pamoja na kufunga kwa pamoja ni katika Bid´ah ambazo zimezushwa na baadhi ya vijana. Hili halina asli. Kila mmoja afunge na kufuturu katika hali yake. Hakuna neno ukafuturu na familia yako na hili sio jambo linaloitwa “kufuturu kwa pamoja”. Kufuturu kwa pamoja ni kule ambako watu wanakusudia kukusanyika. Ama wanafamilia, marafiki na wasafiri kufuturu kwa pamoja, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (46) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-04-01.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014