al-Fawzaan kuhusu du´aa ya al-Mughaamisiy juu ya kudhulumu


Swali: Swaalih al-Mughaamisiy amesema:

“Ukimdhulumu mtu soma du´aa hii: “Ee Allaah! Zile haki ulizo nazo juu yangu nisamehe. Na zile haki za wengine zilizo juu yangu nibebee nazo.””

Swali: Kuna mlinganizi mmoja anayesema kwamba ukimdhulumu mtu soma du´aa ifuatayo: “Ee Allaah! Zile haki ulizo nazo juu yangu nisamehe. Na zile haki za wengine zilizo juu yangu nibebee nazo.”” Je, du´aa hii imewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Ndugu! Ukimdhulumu mtu mrudishie haki yake uliyomdhulumu. Kuomba du´aa peke yake haitoshi. Rudisha vya watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kurudisha haki za watu duniani kabla huko Aakhirah zikaja kuwa dinari na dirhamu. Midhali bado uko hai na una uwezo rudisha haki za watu kwa wenye nazo. Endapo huna uwezo, ni lazima kuomba msamaha na mwenye haki yake akusamehe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=DuSviAcgpJk