Nimesoma kitabu kwa jina ”as-Salafiyyah Marhalah Zamaniyyah Mubaarakah, laa Madhhab Islaamiy” kilichoandikwa na Dr. Muhammad Sa´iyd Ramadhaan al-Buutwit. Nikashangazwa na kichwa cha khabari hicho kinachoashiria kwamba Salaf kuwa na madhehebu yoyote na mfumo ambao ni lazima kwetu kuutambua na  kushikamana nao na sambamba na hilo kuyaacha madhehebu yanayokwenda kinyume nayo. Nilipoanza kusoma kitabu nikaona kuwa yaliyomo ndani yanashangaza zaidi kuliko kichwa cha khabari. Ndani yake amesema kuwa madhehebu ya Salafiyyah ni Bid´ah  na kuwashambulia Salafiyyuun. Nimejiuliza kama mashambulizi yake haya yenye kuenea dhidi ya Salafiyyah na Salafiyyuun – wakiwemo wale wa kale kama mfano wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab – yanatokana na kuchukia kwake Bid´ah na ndipo akafikiria kuwa Salafiyyah ni madhehebu. Kamwe sivyo hivyo! Kilichomfanya sio kuchukia kwake Bid´ah. Kwa sababu tumemuona akisapoti Bid´ah nyingi katika kitabu hichi. Anasapoti Adhkaar za Suufiyyah, du´aa za pamoja baada ya kumaliza kuswali swalah za faradhi, jambo ambalo ni Bid´ah, kufunga safari kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo ni Bid´ah…

Hivyo ikatubainikia – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – kwamba kilichompelekea katika mashambulizi haya ni kuona kwake dhiki dhidi ya rai za Salafiyyah zinazopambana na Bid´ah na fikira ambazo waislamu wengi wa leo wakonazo ambazo haziafikiani na mfumo wa Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´qiybaat ´alaa Kitaab as-Salafiyyah laysat Madhhaban, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 11/04/2020