al-Fawzaan kuhusu arobaini ya kufa kwa maiti


Swali: Sisi katika mji wetu anapokufa mtu kunachinjwa kichinjwa siku ya kufa kwake na nyama hii wanapewa waliokuja kutoa pole na waliohudhuria janaza baada ya kumzika maiti. Je, inajuzu kula katika kichinjwa hichi?

Jibu: Hapana. Hii ni Bid´ah na haijuzu kula katika kichinjwa hichi. Hakikuwekwa katika Shari´ah. Ni Bid´ah na haijuzu kula katika kichinjwa hichi. Kadhalika haijuzu hata katika siku ya arubaini tokea siku ile alipokufa wanachinja na wanaita “kichinjwa cha arubaini“. Kitendo hichi hakijuzu. Ni Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-5-11.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014