Swali: Sauti si nzuri na tumechopata kuelewa kwenye swali ni al-Mawduudiy na vitabu vyake…

Jibu: Sijui kuwa Abul-´Alaa´ al-Mawduudiy (Rahimahu Allaah) ametilia uzito wowote katika kueneza ´Aqiydah. Alitilia umuhimu katika kueneza madhehebu ya al-Ikhwaan al-Muslimuun. Vitabu vyake vyote vinahusiana na hilo. Sijui kuwa ametilia uzito katika kueneza ´Aqiydah, kulingania katika Tawhiyd na kukemea shirki. Siyajui hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/9355
  • Imechapishwa: 03/05/2020