al-Fawzaan kuhusu Aayah ya mwisho kuteremka


Swali: Je, Aayah hii ndio ya mwisho kuteremka katika Qur-aan:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

“Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe (ndio) Dini yenu.” (05:03)

au baada yake kumeteremka kitu? 1,10

Jibu: Allaah ndiye Anajua zaidi. Kwa hali yoyote ni katika Aayah za mwisho zilizoteremka. Wanachuoni wametofautiana ni Aayah ipi ya mwisho kuteremka. Wanasema Aayah ya mwisho kuteremka ni Aayah ya mwisho ya Ribaa, Kauli Yake (Ta´ala):

وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

“Na iogopeni Siku mtayorejeshwa humo kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.” (02:281)

Ni Aayah ya mwisho ya Ribaa. Ama kuhusu Aayah hii:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

“Leo Nimekukamilishieni Dini yenu… “ (05:03)

Ni miongoni mwa Aayah za mwisho zilizoteremka. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuishi baada yake isipokuwa miezi miwili na siku kadhaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 14/11/2014