al-Fawzaan kuhukumiwa na hukumu ya kikafiri

Swali: Nchi yetu inamlazimisha kitu mgonjwa ambaye anataka uchunguzi wa udaktari kupiga saini mkataba pamoja na daktari kabla ya uchunguzi wa daktari. Mkataba unasema kuwa endapo kutatokea malalamiko au tatizo lolote kutoka daktari basi jambo hilo lirejeshwe mahakamani. Je, inajuzu kwa mgonjwa muislamu kupiga saini mkataba huu unaosema mtu ahukumiwe na mahakama ya kikafiri kwa kuzingatia ya kwamba waislamu hawana la kufanya?

Jibu: Haina neno ikiwa mtu hawezi kuifikia haki yake isipokuwa kwa kufanya hivo. Aache haki yake ipotee? Asiache haki yake ipotee. Ikiwa anachukua haki yake peke yake na si ya mwengine ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20-%2024-10-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017