al-Fawzaan: Chanjo dhidi ya uviko-19 ni neema kutoka kwa Allaah

Kwanza tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa neema Zake za wazi na zilizojificha. Kisha tunaishukuru nchi yetu tukufu kwa yale matibabu na utunzaji wanayowafanyia waislamu na sababu nyenginezo zinazosaidia kwa idhini ya Allaah. Hizi ni fadhilah za Allaah juu yetu na kwa watu wengine, lakini watu wengi hawashukuru. Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa usahali huu na uwezekano huu ambao ametuwezesha kuweze kupata sababu zenye manufaa zinazopelekea katika afya njema na usalama. Zote hizi ni sababu na mwenye kuponya ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Tunatumai Allaah atanufaisha kupitia sababu hizi na ailipe serikali yetu yenye busara juu ya yale mambo yote yenye manufaa wanayowafanyia wananchi, khaswa wale wahitaji, na watu wengine wote. Tunawashukuru kwa jitihada hizi nzuri. Tunamwomba Allaah awazidishie uwezekano zaidi na awazidishie mafanikio na msaada. Hapana shaka kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameamrisha kufanya sababu. Lakini hata hivyo watu wasitegemee sababu; wanachotakiwa ni kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?reload=9&v=uHmpPeeGo2A
  • Imechapishwa: 12/05/2021