al-Fawzaan anajuzisha kueneza picha zake katika mitandao ya kijamii?

Swali: Kuna maswali mengi yanayosema kuwa kile kitendo cha kudhihiri makala zako kwenye gazeti zilizo na picha na vilevile wakati wa kutoa mihadhara katika baadhi ya chaneli ni dalili yenye kuonesha kuwa wewe unajuzisha picha?

Jibu: Hii sio dalili. Mimi sikuwaamrisha na wala sikuwatafuta. Wao ndio wenye kunifuata. Walichukua picha ya Shaykh Ibn Baaz ilihali anaharamisha hili na kumkataza mwenye kufanya hivo. Pamoja na hivyo wanamchukua picha katika mikutano na minasaba mbali mbali. Madhambi yanawapata wao. Kuhusiana na sisi haturidhii haya, hatukuwaamrisha nayo na wala hawatutaki ushauri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2121
  • Imechapishwa: 01/07/2020