al-Fawzaan alaumiwa kwa kutokemea makosa ya watawala hadharani

Swali 39: Wako wanaokutia kasoro kwa kutokukemea kwako hadharani ile mikhalafa inayofanywa na nchi. Je, una nasaha zozote za kuwapa watu hawa?

Jibu: Hapana shaka kwamba watawala ni kama wengineo katika watu. Haina maana kwamba wamekingwa na kukosea. Kuwanasihi ni jambo la lazima. Lakini kufanya hivo kwenye vikao na juu ya mimbari kunazingatiwa ni usengenyi ulioharamishwa. Huu ni uovu mbaya zaidi kuliko ule uovu unaofanywa kutoka kwa watawala. Kwa sababu ni kusengenya. Jengine ni kutokana na kwamba linaamsha fitina, kufarikisha umoja na kuathiri usongaji mbele wa Da´wah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 151
  • Imechapishwa: 29/09/2019