al-Fawzaan akikanusha madai kwamba Ibn Baaz anakubali uchawi na anasifia kitabu chake “Iqaamat-ul-Baraahiyn”

Swali: Ni ipi hukumu ya kuagua uchawi kwa kutumia uchawi mwingine mfano wake, kuwaendea, huenda wakanasibisha hilo kwa saini ya Shaykh Ibn Baaz na kwamba jambo hilo lipo katika vitabu vya wanachuoni wa Fiqh na Hanaabilah?

Jibu: Ama kumnasibishia Shaykh Ibn Baaz ni uongo wa wazi. Shaykh Ibn Baaz anafutu juu ya uharamu wa uchawi na kwamba haijuzu kujitibu nao. Ana kijitabu kwa jina “Iqaamat-ul-Baraahiyn”[1] ambapo ndani yake amewaraddi waganga, wachawi na madajali. Ni kijitabu kimeshachapishwa na kinapatikana vilevile katika majibu na fataawa zake (Rahimahu Allaah).

Ni kijitabu kimeshachapishwa na kinapatikana vilevile katika majibu na fataawa zake (Rahimahu Allaah). Kwa hivyo kumnasibishia kauli ya kwamba anajuzisha kuondoa uchawi kwa kutumia uchawi mwingine ni kumsemea uongo Shaykh.

Ama kusema kwamba baadhi ya wanachuoni wa kale wameona kuwa ni jambo linalofaa, itambulike kuwa kila mmoja yanachukuliwa maneno yake na yanarudishwa. Haijuzu kuchukua maoni ya mwenye kujibu pale yanapokuwa yanapingana na Qur-aan na Sunnah na itakuwa sio hoja. Dalili ni yenye kutolewa katika Qur-aan na Sunnah na maafikiano ya waislamu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/wp-content/uploads/2017/01/IQAAMAT-UL-BARAAHIYN_-_IMAAM_IBN_BAAZ__2016_05_09_16_18_08_896.pdf  

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 154 http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 30/12/2018