al-Faqiyhiy kuhusu maulidi

Miongoni mwa Bid´ah hizo ni Bid´ah ya mazazi ya Mtume. Kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo la wajibu kwa kila muislamu. Imani ya muislamu haitimii mpaka Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) awe ni mwenye kupendwa zaidi kwake kuliko anavyojipenda mwenyewe, mtoto wake, baba yake na watu wote kwa jumla. Haya yamepokelewa katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy.

Lakini hata hivyo kumpenda kunakuwa kwa kumtii na kumfuata. Kwa msemo mwingine ni kwa kutekeleza maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amekataza Bid´ah bali na kuitahadharisha pale aliposema:

“Kila Bid´ah ni upotevu.”

“Atakayetenda kitendo ambacho hamna ndani yake dini yetu, basi atarudishiwa mwenyewe.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Haikuthibiti kwake yeye, makhaliyfah wake, Maswahabah zake na wale wanachuoni wenye kustahiki kufuatwa yeyote ambaye alifanya maulidi. Uhakika wa mambo ni kwamba maulidi haya yalizushwa na al-Faatwimiyyuun al-´Ubaydiyyuun ambao walikuwa ni Raafidhwah. Wanajinasibisha na Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ilihali uhakika wa mambo walikuwa ni mayahudi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bid´ah – Dhwawaabitwuhaa wa atharuhaa as-Sayyiu´ fiyl-Ummah, uk. 18
  • Imechapishwa: 27/08/2020