al-Faatihah wakati wa kusahau kitu

Swali: Baadhi ya watu wanaposahau kitu au wanapotaka kitu wanasoma Suurah “al-Faatihah”. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni Bid´ah. Bali ni lazima kwake kumtaja Allaah kama kusema “Hapana mwabudi wa haki isipokuwa Allaah”, “Subhaan Allaah” na mfano wake. Amesema (Ta´ala):

وَاذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ

“Mtaje Mola wako unaposahau. “[1]

[1] 18:24

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 72
  • Imechapishwa: 21/07/2019