Baadhi wanasema kwamba al-Awzaa´iy alisema kuhusiana na Hadiyth:

“Mola wetu (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka katika mbingu ya chinu ya dunia pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na anasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie? Ni nani aniulizaye nimpe?”

“Allaah anafanya atakavyo.”

Wanamaanisha kwamba alifasiri ushukaji kwamba ni kitendo miongoni mwa vitendo Vyake kinachotokea kupitia uwezo Wake. Haijuzu kusema kwamba amefasiri kushuka kwa Allaah kwamba ni katika sifa Zake za kimatendo. Kwani hakusema wazi hapo. Jengine ni kwamba tumepokea kutoka kwa Salaf kuwa wamesema kitu kingine kisichokuwa hicho.

  • Mhusika: Imaam Abu Ya´laa Muhammad bin al-Husayn al-Farraa’
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ibtwaal-ut-Ta’wiyl (1/57-58)
  • Imechapishwa: 08/02/2019