Swali: Unamjua mpotevu huyu Haatim ash-Shariyf au sijui anaitwaje. Siku hizi amekuwa ni mwenye kuitukana ”ad-Durar as-Saniyyah” na anadai kuwa ndio msigni wa Takfiyr. Anamtuhumu Shaykh Aba Butayn na Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kwamba ni Khawaarij. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Yule ambaye anawatukana [sauti haiko wazi] maimamu wa Da´wah ni dalili yenye kujulisha kuwa moyoni mwake mna maradhi. Wanachuoni wameshimiwa wanatambua fadhilah walizonazo maimamu wa Da´wah [sauti haiko wazi]… Yule mwenye kumtukana na kumponda Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab  ni dalili inayojulisha kwamba moyoni mwake mna maradhi.

Swali: Unawanasihi nini juu ya ash-Shariyf huyu. Mtu huyu anamshambulia Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab  na maimamu wa Najd na ”ad-Durar as-Saniyyah”.

Jibu: Yule mwenye kuwatukana wanaume hawa, ni mamoja yeye au wengine, hapana shaka kwamba  [sauti haiko wazi]. Mtu kama huyo haitakiwi kuchukua faida kwake, kwa sababu moyoni kwake mna maradhi. Yule mwenye kumtukana Shaykh Aba Butayn, maimamu wa Da´wah au Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab moyoni mwake mna maradhi, ni mamoja kama yeye au mwenginewe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=2Co1X0AXUjw&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 20/03/2020