al-Albaaniy ni imamu wa Ahl-us-Sunnah


Pindi nilipokuwa nazungumzia mwenendo wa wapindaji ambao wameshikamana na maandiko yasiyokuwa wazi ya mwanamke [… sauti haiko wazi… ] kuhusu Hijaab baadhi ya watu wakasema kuwa nakusudia Shaykh al-Albaaniy na kwamba ni katika watu waliopinda. Ninamuomba Allaah usalama na afya. Shaykh al-Albaaniy ni imaam miongoni mwa maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na ni mwanachuoni wa Hadiyth. Vipi mtu anaweza kusema namkusudia Shaykh al-Albaaniy? Ni tafsiri aina gani hizi za kimakosa? Ninawanasihi vijana kuacha na dhana hizi na tafsiri kama hizi za makosa.

Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) ni mwanachuoni wa Hadiyth wa zama hizi. Ameitumikia Sunnah na kutunga vitabu vikubwa na ukaguzi wa vitabu. Vipi mtu pindi ninapozungumzia wapindaji mtu anaweza kusema kuwa namkusudia Shaykh al-Albaaniy?

Ni wajibu kwa vijana wamche Allaah. Watambue kuwa wanapata dhambi kwa kufanya hivi. Haijuzu kwao kuzungumza maneno aina hii.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/AbdelazizRajhi/divers/21_arba.mp3
  • Imechapishwa: 06/09/2020