Swali 1117: Ni ipi hukumu ya mwanamke kupunguza nywele zake?

Jibu: Mwanamke kukata nywele zake kutatazamwa kilichompelekea katika kitendo hicho. Ikiwa mwanamke anapunguza nywele zake kwa ajili ya kujifananisha na wanawake wa kikafiri au wanawake waovu, basi haitofaa kukata nywele zake kwa nia hiyo. Ama ikiwa mwanamke anapunguza kwa kukhafifisha nywele zake au kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya mume wake, basi sioni juu ya hilo kizuizi midhali imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim ya kwamba wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakipunguza nywele zao mpaka zikawa kama kitu kilichokusanywa[1].

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema akimnukuu Shaykh Muhammad al-Aamiyn ash-Shanqiytwiy (Rahimahu Allaah) katika “Adhwaa´-ul-Bayaan:

”Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walipunguza nywele za vichwani mwao baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu walikuwa wakijipamba wakati wa uhai wake na miongoni mwa mapambo yao makubwa ni pamoja na nywele zao. Lakini baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wana hukumu ambazo ni maalum kwao pekee wasizoshirikiana na mwanamke yeyote katika wanawake wa ulimwenguni. Hukumu yenyewe ni kukatika kwa matarajio na tamaa ya kuolewa ambayo haikuchanganyikana na tamaa yoyote. Wao ni kama wenye eda wenye kufungwa kwa sababu yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka pale watapokufa.” Tazama “Tanbiyhaat ´alaa Ahkaam Takhtasswu bil-Mu´minaat”, uk. 18-19

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 451
  • Imechapishwa: 13/10/2019