al-Albaaniy mkono wa kutumia wakati wa kupiga Siwaak

Swali 357: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak? Muislamu atumie mkono gani?

Jibu: Siwaak ni Sunnah iliyokokotezwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth nyingi. Kuhusu mkono wa kutumia hakuna andiko la wazi tunalotegemea.

Wako wanachuoni wanaosema mkono wa kuume na wengine wanasema mkono wa kushoto. Lakini katika maoni mawili hayo yako ambayo yana mtazamo; wale wanaosema mkono wa kuume wanatendea kazi kuanza kutumia upande wa kuume katika kila jambo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 138
  • Imechapishwa: 27/09/2019