Wakomunisti wameweka hadharani fikira yao: Uislamu hausilihi. Kila ambaye analianika hilo hadharani ni kafiri na mwenye kuritadi. Hapana shaka yoyote juu ya hili kwa sababu ni ukafiri wa kiitikadi.

Ikiwa watawala hawa waliopinda – bila kujali wamepinda sana au kidogo –  watazungumza kwa njia itayotufanya kwamba lipo jambo ambalo halisilihi katika Uislamu hii leo, basi wanajiweka wenyewe katika kuritadi kwa wazi. Yule mwenye kuonelea hivo – pasi na kujali ni kiasi gani – basi ameritadi kutoka nje ya dini yake.

Ama ikiwa tu wanahukumu kwa kanuni ambazo msingi wake sio za Kiislamu – au zote kabisa – basi inazingatiwa kuwa ni kufuru ya kimatendo. Ni lazima kuwepo ushahidi kwamba ni kufuru ya kiitikadi. Kwa ajili hiyo mimi siwatazami kwa mtazamo mmoja chama cha Ba´th, au wakomunisti, wanaosema kuwa Uislamu umekuja kwa waarabu na kwamba tarehe yake imekwisha. Lakini kuna watawala wengi ambao hawaonyeshi jengine isipokuwa tu kujali kwao kiti na kuwatawala watu. Huu ni msiba, lakini mimi sioni kuwa jambo hilo ni kufuru ya kiitikadi. Kama kuna ambaye anaonelea hivo basi tunamuomba atubainishie ili tuweze kukurubiana fahamu na kuelewana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1003) Tarehe: 1410-01-19/1989-08-21
  • Imechapishwa: 16/10/2020