Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Kaka yake na Sayyid Qutwub Muhammad [Qutwub] ndio ambaye ana jukumu la kuhakiki kitabu chake “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na kunachapishwa mamilioni ya matoleo. Nilimpigia simu na kumwambia kuwa yeye ndiye mwenye jukumu la “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na matoleo yake. Nikamuuliza kwa nini haweki taaliki kwenye “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”. Akanijibu kuwa habadili kitu na wala hatogeuza kitu. Nikamwambia kuwa mimi sikuombi ubadili wala ugeuze kitu, lakini ninachokuomba ni kuweka taaliki kwa kujisalimisha na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuona maovu katika nyinyi, badi ayabadilishe [ayaondoshe] kwa mkono wake. Na ikiwa hatoweza, ayabadilishe kwa mdomo.” (Muslim (49))

Nikamwambia anachoweza kufanya ni yeye kuandika taaliki na kuashiria Wahdat-ul-Wujuud katika Suurat-ul-Haadiyd na kwa mfano kuandika:

“Hapa kaka yangu alikosea. Hili ni kosa. Hii ni Wahdat-ul-Wujuud ya Suufiyyah inayopingana na Tawhiyd.”

na mfano wa hivo. Akanyamaza, halafu akasema:

“Allaah Akujaze kheri kwa bidii yako.”

al-Albaaniy: Hivo tu?

Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Ndio. Nikamuomba afanye hivo na kunitumia nuskha ilio na taaliki. Hii ni nasaha kwa wale waliohai ambao wamejipa jukumu la kueneza vitabu vyake.
al-Albaaniy: Je, kuna maoni tofauti juu ya hili?

Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Hapana, hakuna – Allaah Akitaka.

al-Albaaniy: Hili ndilo tunalosema. Kama jinsi unavojua ni kwamba mtu wa kwanza kumraddi Sayyid Qutwub juu ya Wahdat-ul-Wujuud ni mtu huyu ambaye wewe hivi sasa unazungumza naye. Kisha akaraddiwa kwenye gazeti la “al-Mujtamaa´” chini ya anuani:

“Shaykh al-Albaaniy anamkufurisha Sayyid Qutwub”

Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Ilikuwa ni ´Abdullaah ´Azzaam ndio aliandika hivo. Sisi hatumkufurishi. Isitoshe Muhammad Qutwub anasema katika kitabu “Laa ilaaha illa Allaah” ya kwamba mapungufu ni katika maumbile ya mwanaadamu na kuwa Aadam pia alikosea. Akatumia hoja Aayah:

وَعَصَىٰ آدَمُ رَبَّهُ فَغَوَىٰ

”Aadam akamuasi Mola Wake akapotoka.” (20:121)

Nikamwambia ya kwamba Allaah Amesema:

وَلَقَدْ عَهِدْنَا إِلَىٰ آدَمَ مِن قَبْلُ فَنَسِيَ وَلَمْ نَجِدْ لَهُ عَزْمًا

”Kwa hakika Tulimpa Aadam ahadi kabla, lakini akasahau na wala hatukuona kwake azimio.” (20:115)

Je, Aadam alikosoea kuhusiana na maamrisho ya Shari´ah?

al-Albaaniy: Nimeshawaambia ya kwamba watu hawa sio wanachuoni. Wanachuoni wenyewe wakati mwingine hawawezi kujieleza kwa njia ya sawa. Wanachuoni ambao ni wajuzi zaidi kuliko sisi wakati mwingine hawawezi kujieleza kwa njia ya sawa. Watu hawa ni waandishi tu na sio wanachuoni.

Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Hata hivyo ni lazima kuwanasihi.

al-Albaaniy: Kwani mimi nimekwambia usiwanasihi?

Shaykh Muhammad bin Jamiyl Zaynuu: Hapana. Wanahubiri kwenye chuo kikuu. Wanawaandikia watu na watu wanawaamini. Ni wajibu kwetu kuwabainishia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (915)
  • Imechapishwa: 26/08/2020