al-Albaaniy kuhusu mtoto wa chupa (test tube)

Swali 746: Inajuzu kwa mwanaume kumruhusu daktari manii yake kwenda kwa mke wake au kile kinachotambulika kama “mtoto wa chupa” (test tube)?

Jibu: Haijuzu. Kwa sababu uhamishaji huu unapelekea angalau kwa uchache daktari kufunua uchi wa mke. Kufunua nyuchi za wanawake ni jambo lisilojuzu Kishari´ah. Haijuzu kufanya jambo hilo isipokuwa kwa dharurah. Hatufikirii kuwa kuna udharurah kwa mwanaume kuhamisha manii yake kwenda kwa mke wake kwa njia kama hii.

Mara nyingine jambo hili hupelekea daktari kufunua uchi wa mwanaume pia, jambo ambalo halijuzu. Kupita mapito kama haya ni kuwaigiliza wamagharibi katika kila kile wanachokileta.

Mtu huyu ambaye hakuruzukiwa mtoto kwa njia ya kimaumbile maana yake ni kwamba hakuridhia mipango na makadirio ya Allaah. Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewahimiza waislamu kupita njia inayokubalika Kishari´ah katika jambo la kutafuta riziki na chumo halali, basi ni jambo lina haki zaidi kuwahimiza kupita njia inayokubalika Kishari´ah katika jambo la kumpata mtoto.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 291
  • Imechapishwa: 20/09/2019