Muulizaji: Katika moja ya miji ya Uholanzi kuna genge limekuja na fikira ambayo kutokana na vile tunavojua inatokea Misri, nayo ni Jamaa´at-ut-Takfiyr wal-Hijrah.

al-Albaaniy: Jamaa´at-ut-Takfiyr wal-Hijrah, ndio. Wamefika Algeria.

Muulizaji: Katika moja ya miji ya Uholanzi kuna genge ambalo haliswali misikitini. Wanawakufurisha wengine na kukiwemo hata Salafiyyuun wanaoswali nyuma ya imamu huyu. Wanasema kuwa ni mzushi na kadhaa na kadhaa…

al-Albaaniy: Tatizo la watu hawa ni khatari zaidi kuliko yale uliyoyataja kwamba hawaswali katika misikiti ya waislamu. Sababu ya kutokuswali kwao nyuma ya maimamu hawa sio kwa sababu eti wanaona kuwa maimamu si wenye ikhlaasw kwa vile wanawaswalisha watu kwa mkabala wa mshahara wao au kwa sababu kuna wazushi wengi katika misikiti hiyo. Si hilo tatizo. Tatizo ni kwamba wanawaona kuwa ni makafiri.

Wanaona kuwa waislamu katika miji ya waislamu, sembuse Uholanzi, Polen na miji mingine ya kikafiri, ni makafiri. Wanaona kuwa wote hao ni makafiri kuanzia kwa mtawala mpaka mwananchi. Wanatumia juu yao maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (al-Maaidah 05:44)

kwa watawala wote katika miji ya waislamu. Hawatofautishi kati ya yeyote miongoni mwao. Kisha wanatumia hukumu hiyohiyo juu ya mlinzi wa msikiti na si kwa muadhini wala imamu peke yake. Kwa nini wanafanya hivo? Kwa sababu wanamsapoti mtawala na wanaridhia hukumu yake. Hivyo matokeo yake wanawaweka wote katika hukumu moja, kuanzia kwa mtawala mpaka kwa raia, na kuwaona wote kuwa ni makafiri. Kwa ajili hiyo ndio maana hawaswali [misikiitini] na sio kwa sababu eti ya Bid´ah, kasoro katika ikhlaasw na mfano wa hayo.

Hili si jipya. Sisi pia tumepewa mtihani hapa kwa vijana ambao tulifikiri kuwa wako pamoja nasi, kutokana nasi na kati yetu. Nilishangazwa nao kwa sababu walikuwa wakijengea hoja kwa vitabu vyangu na wakinufaika kwavyo, kitu ambacho walikuwa wakikifanya kwa uwazi. Tulikutana na baadhi yao hapa. Wakakataa kuswali swalah ya ijumaa na swalah ya mkusanyiko. Hawaswali kabisa kutokana na sababu niliyokutajia punde kidogo. Kosa lao laanza kutokea katika Aayah tukufu kwa vile wameifahamu ufahamu wa kimakosa. Hilo likafuatiwa na makosa mengine mengi. Miongoni mwa makosa hayo ni kwamba wanakosoa upokezi wa Ibn ´Abbaas wakati alipofasiri Aayah hiyo na akasema:

“Ni kufuru ndogo.”

Wanasema kuwa upokezi huu sio sahihi. Watu hawa ni wajinga. Hawajui elimu ya Hadiyth wala elimu ya Jarh wa Ta´diyl. Dini yao si jengine isipokuwa ni matamanio yao. Ni kama ambavo walivokuwa Khawaarij wa kale. Kile kilichowapendeza ndio dini yao. Kile ambacho hakikuwapendeza basi wanakikataa na kukitupilia mbali.

Tunaweza kupata watu wenye ikhlaasw katika watu hawa, lakini hata hivyo ni wapotofu kwa sababu wanatembea pasi na elimu. Wanahitajia wanachuoni wataowashika mkono.

Pindi mtu atapojadiliana nao, basi anatakiwa kuanza juu ya kuwakufurisha kwao waislamu. Kama nilivyokwambia, Ahl-ul-Ahwaa´ wanachukua yale maandiko ya Qur-aan na Sunnah yanayowapendeza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (524)
  • Imechapishwa: 29/05/2021