al-Albaaniy anafahamu Hadiyth na hafahamu siasa

Swali: Makundi yanawalazimisha baadhi ya watu kusoma kitabu “Fusuul min as-Siyaasah ash-Shar´iyyah” cha Shaykh ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq na “al-Muslimuun wal-´Amal as-Siyaasiy.” Katika baadhi ya vitabu hivi Shaykh ´Abdur-Rahmaan anasema kuwa hakuna haja kwa mtu kutendea kazi kwa baadhi ya maandiko ya Qur-aan na Sunnah ikiwa mtu anataka kufikia maslahi ya kishari´ah. Vijana wengi Salafiyyuun wa kisudani wamepewa mtihani kwa vitabu hivi. Baadhi yao wamepetuka kiasi cha kwamba, mtu akisema kuwa Shaykh al-Albaaniy amesema kadhaa, wanawavamia wanachuoni wa Hadiyth na kusema:

“Wanakaa hali wamejifungia [milango] na kufundisha, kurekebisha na kusahihisha. Ama kuhusiana na mtu huyu, anasoma hali ya sasa na hili ndio tunalihitajia hii leo. Anatoa maelekezo kwa yale Sudan inayohitajia.”

Mambo yakaishia baadhi wakafikiria kuwa ameandika kitabu hichi khaswa kwa ajili ya Sudan. Kuanzia mwaka wa 84 ghasia hii imepatikana.

al-Albaaniy: Ni jambo lenye kusononesha sana. Haya yanatilia nguvu yale niliyosema na kwamba wenye kuwaongoza vijana wa leo wao wenyewe ni vijana ambao hawajakomaa kielimu.

Ni kweli kwamba al-Albaaniy anasahihisha Hadiyth na kuzidhoofisha, lakini haishi nyuma ya boya kabisa. Anajua yanayoendelea kwa Waislamu. Hata hivyo anashikamana na hukumu za Kishari´ah na haonelei inajuzu kwa Muislamu kusema kuwa lengo linahalalisha njia.

´Abdur-Rahmaan mwenyewe akiulizwa, ambaye alikuwa mwanafunzi wangu kwenye chuo kikuu cha Kiislamu, angelipata swali hili au ningelibahatikiwa kumuuliza swali hili na kama anaonelea kuwa lengo linahalalisha njia, angelisema hapana. Kwa sababu ni kanuni ya kikafiri. Lakini tukimwangalia jinsi yeye na maisha yake yamejengeka juu yake na jinsi anavyohalalisha baadhi ya vilivyo haramu, tutaona jinsi anavyohakikisha kanuni hii ambayo haiwezi kukubaliwa na Muislamu yeyote. Lakini kuna faida gani ya kusema kitu na kufanya kitu kingine?

Kwa hivyo tunajiombea wenyewe na ndugu zetu na watu mfano wake uongofu na mafanikio ili tuweze kufuata kikweli kweli Qur-aan na Sunnah kutokana na mfumo wa Salaf-us-Swaalih.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (402)
  • Imechapishwa: 14/07/2020