al-´Abbaad kuhusu maandamano ya amani


Swali: Mimi natokea Libya na watu wamepanga siku ya jumanne au alkhamisi kutoka nje ya kwa ajili ya maandamano kwenye mabarabara. Tunaomba nasaha na ubainifu kutoka kwako juu ya hukumu ya maandamano na migomo ambavyo wanaita kwamba eti ni vya amani. Huenda Allaah akanufaisha watu kwa nasaha hizi.

Jibu: Sijui chochote kinachofahamisha juu ya uwepo katika Shari´ah kwa maandamano haya. Hatujui msingi katika dini unaofahamisha juu ya mambo haya. Ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa yaliyozuliwa na watu na ambayo wameyatoa kutoka kwa maadui wao na kutoka katika nchi za magharibi na mashariki. Hayana msingi katika dini. Hatujui kitu kinachofahamisha juu ya kufaaa kwake na juu ya uwepo wake katika Shari´ah. Kwa ajili hii watu wanapaswa kupita mapito ya Kishari´ah waliyowekewa na waachane na mambo yasiyokuwa na msingi wowote na isitoshe yanapelekea katika madhara, uharibifu, mauwaji na unyonge. Miongoni mwa madhara yake kama kusingelikuwa zaidi ya kuwapa dhiki watu katika barabara na njia zao basi ingelikuwa inatosha katika kubainisha ubaya wake na kwamba haifai kwa yeyote kufanya mfano wa mambo haya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 17/11/2019