Ajiunge na imamu au asubiri mkusanyiko wa pili?

Swali: Je, mtu ajiunge pamoja na imamu akiingia msikitini na akamkuta imamu katika Tashahhud ya mwisho au asubiri ili aweze kuswali na mkusanyiko mwingine akiwa na yakini juu ya uwepo wao?

Jibu: Kusipokuweko watu basi ajiunge na mkusanyiko ulioko sasa. Lakini kukiweko watu wengine basi yuko na khiyari; akitaka atajiunga pamoja na imamu na akitaka atasubiri mpaka atoe Tasliym na baada ya hapo wataswali. Swalah itakuwa imekwisha na hakukubaki kitu. Lakini aliyechelewa akiwa ni mmoja tu basi ajiunge pamoja na imamu.  Kule kutarajia kwake atakuja mtu pengine matarajio yake haya yasitimie.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 11/06/2021