Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mwenye furaha ni yule aliyefurahishwa kwa aliyopanga Allaah na aliye na khasara ni yule aliyekhasirishwa kwa yale aliyopanga Allaah.”

Kwa sababu furaha imeandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa. Kadhalika kila mtu kama ilivo katika Hadiyth ya Ibn Mas´uud iliyotangulia anapokuwa tumboni mwa mama yake anapuliziwa pumzi na kunaandikwa kama atakuwa mwenye furaha au mwenye khasara. Haya yanakuwa ni yenye kuafikiana na yaliyomo katika Ubao Uliohifadhiwa. Kwa sababu asli ni yale yaliyoandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa. Furaha au khasara yote yameandikwa katika Ubao Uliohifadhiwa. Haya ni makadirio ya jumla yaliyoko kwenye Ubao Uliohifadhiwa ambapo kumeandikwa ndani yake kila kitu:

وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ

“Na kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari lenye kubainisha.” (36:12)

Kisha kuna makadirio ya umri kwa kila mtu anapokuwa tumboni mwa mama yake kunaandikwa kama atakuwa mwenye furaha au khasara, matendo, riziki na muda wake ataoishi.

Halafu kuna makadirio ya mwaka. Nayo ni yale yanayokuwa katika usiku wenye cheo (Laylat-ul-Qadr). Allaah huandika yatayokuwa katika mwaka huo; mauti, uhai, madhalilisho, utukufu, khasara na furaha.

Kisha kuna makadirio ya kila siku. Nayo ni yale makadirio anayokadiria Allaah kwa yanayokuwa kila siku. Allaah (Ta´ala) amesema:

كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ

“Kila siku Yeye Yumo katika kuleta jambo.” (55:29)

Anatukuza, anadhalilisha, anaumba, anahuisha, anafisha, anafanya kupatikana furaha au khasara, anafanya kupatikana ufuraha au utajiri (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/366-367)
  • Imechapishwa: 21/05/2020