Swali: Mtu anaweza kuwa walii wa Allaah ilihali hatendei kazi Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Inategemea na ni matendo yepi aliyoacha. Mtu anaweza kuwa na sehemu ya mapenzi ya Allaah na sehemu ya uadui. Watenda madhambi na watu wa madhambi makubwa wana mapenzi ya Allaah kwa sababu ya shahaadah, Tawhiyd na ´Aqiydah sahihi. Lakini wana uadui vilevile kwa sababu ya maasi na madhambi makubwa. Mtu anaweza kukusanya kati ya mapenzi na uadui. Kama ilivyotangulia kuna ambao ni mawalii safi. Wengine ni maadui wa Allaah safi. Wengine wamekusanya yote mawili. Hili linatofautiana kutegemea na yale matendo aliyoacha na yale maasi anayofanya. Kama mnavyojua imani inazidi na kupungua. Inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (04) http://alfawzan.af.org.sa/node/2047
  • Imechapishwa: 05/11/2016