Tatizo sio ule ujinga mwepesi. Tatizo ni kwa yule ambaye ni mjinga asiyejitambua. Ni yupi huyu? Ni yule asiyejua na wala hajui kuwa hajui. Kwa ajili hii nitawapa mifano mitatu za ambaye ni mjinga na mjuzi:

1- Mtu wa kwanza aliulizwa vita vya Badr vilikuwa lini ambapo akajibu ya kwamba ilikuwa katika mwaka wa pili.

2- Mtu wa pili aliulizwa vita vya Badr vilikuwa lini ambapo akajibu ya kwamba ilikuwa katika mwaka wa nne.

3- Mtu wa tatu aliulizwa vita vya Badr vilikuwa lini ambapo akajibu ya kwamba yeye hajui.

Mtu wa kwanza ambaye amesema kuwa vita vya Badr vilikuwa mwaka wa pili ndiye mjuzi.

Mtu wa pili ambaye amesema kuwa vilikuwa katika mwaka wa nne ujinga wake ni wa kutojijua.

Mtu wa tatu ambaye amesema kuwa hajui ujinga wake ni mwepesi. Mtu mwenye ujinga huu ni bora kuliko yule amabye hajijui kuwa ni mjinga. Kwa sababu mtu wa sampuli hii hujikweza na hujiona kuwa ni msomi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/730
  • Imechapishwa: 25/11/2017