Suurah hii, pamoja na ufupi wake, imekusanya mambo ambayo haijakusanya Suurah yoyote ndani ya Qur-aan. Imekusanya aina tatu za Tawhiyd:

1- Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ambayo inachukuliwa kutoka katika maneno Yake:

رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Mola wa walimwengu.”

2- Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah ambayo ni kule kumpwekesha Allaah kwa ´ibaadah. Inachukuliwa katika maneno Yake:

اللَّهِ

”Allaah.”

pia:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

”Wewe pekee ndiye tunakuabudu.”

3- Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat. Ni kule kumthibitishia Allaah sifa kamilifu ambazo amejithibitishia Mwenyewe na akamthibitishia Mtume Wake. Mtu anatakiwa kufanya hivo pasi na kukanusha, kufananisha wala kushabibisha. Dalili ya hilo ni tamko lake:

الْحَمْدُ

“Himdi.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 28
  • Imechapishwa: 02/05/2020