Aina tatu za subira katika swawm

Swali: Je, kufunga kunazingatiwa ni kuwa na subira?

Jibu: Hapana shaka. Wamesema kuwa subira imekusanya aina tatu za subira:

1- Subira juu ya makadirio ya Allaah.

2- Subira juu ya yale Allaah aliyoharamisha.

3- Subira juu ya utiifu wa Allaah.

Yote haya yanapatikana katika swawm. Ni kumtii Allaah, ndani yake kuna subira juu ya makadirio ya Allaah yenye kuumiza kutokana na ile njaa na kiu anachopata na pia ni kusuburi juu ya yale Allaah aliyoharamisha kwa njia ya kwamba anaizuia nafsi yake na yale mambo yanayofunguza kama vile maji na pengine wakati huohuo ni mwenye kiu na chakula pengine wakati huohuo ni mwenye njaa. Anaizuia nafsi yake. Hii ni dalili inayothibitisha imani yake. Akitaka anaweza kula na kunywa pasi na yeyote kujua. Lakini kule kumuamini kwake Allaah kunamzuia juu ya hilo hata kama atakuwa peke yake mahali na gizani na hakuna yeyote anayemwona. Mtu huyu hawezi kuyaendea maasi ya Allaah. Imani yake ndio inayomzuia kutokamana na hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (80) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-17-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 09/11/2018