Swali: Jirani kafiri ni lazima kumtendea wema?

Jibu: Ndio. Ni lazima kumtendea wema jirani kafiri japokuwa ni kafiri[1]. Inahusiana na haki ya ujirani. Kuna majirani aina tatu:

Ya kwanza: Jirani ambaye ana haki tatu.

Ya pili: Jirani ambaye ana haki mbili.

Ya tatu: Jirani ambaye ana haki moja.

Jirani ambaye ana haki tatu ni yule ambaye ni ndugu na muislamu. Ana haki ya ujirani, ya udugu na haki ya Uislamu.

Jirani ambaye ana haki mbili ni yule ambaye ni muislamu lakini hata hivyo sio ndugu. Huyu ana haki ya ujirani na haki ya Uislamu.

Jirani ambaye ana hakih moja. Huyu ni yule jirani ambaye ni kafiri.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/msimamo-wa-muislamu-kwa-jirani-yake-ambaye-ni-kafiri/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (74) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-25-01-1439H-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/11/2017