Swali: Ni ipi hukumu ya kumuuliza mpiga ramli?

Jibu: Kumuuliza mpiga ramli kumegawanyika aina tatu:

Ya kwanza: Akamuuliza na akamsadikisha. Hili linahesabika ni haramu. Bali ni kufuru. Kwa sababu kumsadikisha katika mambo yaliyofichikana ni kuikadhibisha Qur-aan.

Ya pili: Akamuuliza ili ampime kama ni mkweli au mwongo. Lengo sio ili aweze kuyachukua maneno yake. Hili linafaa. Mtume alisema kumwambia Ibn Sayyaad: “Nimekuficha nini?” Akasema: “ad-Dakhu.” Ndipo akasema: “Koma! Huwezi kuvuka zaidi ya ngazi ulio nayo.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza kitu kwa lengo amjaribu na sio kwa sababu amsadikishe na kuyapokea maneno yake.

La tatu: Akamuuliza ili kudhihirisha kutokuweza kwake na uongo wake. Hili ni jambo linalotakikana na la wajibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/183)
  • Imechapishwa: 10/07/2017