Swali: Kuna wanaosema kuwa imani ni aina tatu:

1 – Imani ya nguzo. Nayo ni kuamini mambo ya nguzo.

2 – Imani ya wajibu. Nayo ni kuamini mambo ya wajibu.

3 – Imani iliyopendekezwa. Nayo ni kuamini mambo yaliyopendekezwa.

Yule asiyeamini mambo yaliyopendekezwa haimdhuru imani yake chochote. Ni ipi hukumu ya msemo huu?

Jibu: Haya ni ya kwake yeye. Ni maneno yenye kichwa chini miguu juu. Hayakusemwa na Salaf wa Ummah na maimamu wake. Vigawanyo hivi havina asli na wala havina dalili.

Mimi nimeshawaambia tokea mwanzo: acheni mambo haya na someni vitabu vya Salaf. Someni vitabu vya ´Aqiydah sahihi na kuwa ngangari kwavyo na acheni kujikakamua huku na maneno haya. Haya ni maneno ya kijinga. Haya ni maneno ya kijinga na ya wenye kujifanya ni wanachuoni. Achaneni nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_08.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2018