Swali: Je, rehema ni sifa ya kidhati ya Allaah au ni sifa ya kimatendo?

Jibu: Allaah ni mwenye kusifika kuwa na huruma. Kuna aina mbili ya rehema:

1 – Kuna rehema ambayo ni sifa miongoni mwa sifa Zake (´Azza wa Jall).

2 – Rehema ya viumbe. Kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Allaah ameumba rehema mia moja na akateremsha kwa watu wa ulimwenguni rehema moja na kwayo ndio watu huhurumiana kiasi cha kwamba [unamuona] mnyama ananyanyua kwato zake asimkanyage mtoto wake kwa kuchelea asije kumuumiza. Itapokuwa siku ya Qiyaamah, basi ataichukua na kukamilisha kwayo mia moja ambapo atawahurumia viumbe.”

Allaah (Ta´ala) ni mwingi wa huruma. Haitakiwi kusema kuwa kuna mara anakuwa na huruma na wakati mwingine anakuwa hana huruma. Kwa sababu ni miongoni mwa sifa za Allaah za kidhati.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 22/01/2022