Aina mbalimbali za Qaz´ na hukumu zake

Swali: Ni ipi hukumu ya Qaz´?

Jibu: Qaz´ ni kunyoa sehemu ya kichwa na kuacha sehemu nyingine. Imegawanyika aina mbalimbali:

Ya kwanza: Akanyoa sehemu ya kichwa pasi na kupangilia. Kwa mfano akanyoa upande wa kulia, kwenye kona na upande wa kushooto.

Ya pili: Akanyoa katikati ya kichwa na akaacha upande wake.

Ya tatu: Akanyoa upande wa kichwa na akaacha katikati yake. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hivyo ndivyo wanavyofanya wapumbavu.”

Ya nne: Mtu akanyoa kwenye kona na akaacha zilizobaki.

Qaz´ aina zote hizi imechukizwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona kijana aliyenyoa sehemu ya kichwa chake tu ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuamrisha ima azinyoa zote au aziache zote. Lakini hata hivyo ikiwa Qaz´ ni yenye kufanana na makafiri inakuwa haramu. Kwa sababu imeharamishwa kwa mtu kujifananisha na makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/118)
  • Imechapishwa: 28/06/2017