Unasema kwenye barua yako:

“Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye.”

Nimeshakubainishia sababu ya yote hayo licha ya kwamba Salafiyyuun hawakunyamazia batili na himdi zote ni Zake Allaah. Daima wameraddi makundi ya batili kadri na wanavoweza. Hii leo khaswa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz ambaye amefanya hivo. Baada ya hapo ni baraza na Kibaar-ul-´Ulamaa´. Yule mwenye kupitia kurasa za Fataawaa za Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz, basi ataona ni Ruduud ngapi alizowapiga watu wa batili. Vivyo hivyo baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa´. Maneno yako:

“Lakini tokea miaka saba ya nyuma ndugu wengi wamemshambulia na kumpokonya haki yake. Haieleweki kabisa. Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye.”

haina maana hakuwaraddi. Haya ni maneno yasiyostahiki. Wanachuoni hawahoji namna hii. Hoja zao kwa yale wanayoyathibitisha na kupinga yale wanayopinga inakuwa kwa Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf.

Ee ndugu mpendwa! Ikiwa unaona kuwa ni mashambulizi kwa Hasan al-Bannaa na mfumo wake na wafuasi wake mtu akimraddi na wafuasi wake wanaotendea kazi Suufiyyah na shirki na kuzusha Bid´ah na kuweka katika Shari´ah mambo ambayo hayakuweka Allaah katika Kitabu Chake wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye Sunnah zake, basi hatuwezi kukuongoza. Pamoja na hivyo tunatakiwa kukuombea kwa Allaah (´Azza wa Jalla) akuondoshe katika fikira yako hii ya ajabu na ufahamu wako wenye kubabaisha ambao umekufanya ukayachanganya mambo. Wakati huohuo tunachelea fikira hizi kukufanya ukaingia ndani ya Aayah:

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا

“Na atakayempinga Mtume baada ya kuwa umeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, basi Tutamgeuza alikogeukia na [baada ya hapo] tutamuingiza Motoni – na uovu ulioje marudio ya mwisho!”[1]

Utambue kwamba kuwa na mapenzi na kuwatetea watu wa batili sio katika njia ya waumini ni mamoja ikiwa ni washirikina au watu wa Bid´ah waliotoka katika Uislamu au ambao hawakutoka. Mimi nakunasihi, ee ndugu yangu, kumuomba Allaah akurejeshe katika haki na kuinusuru. Tunamuomba Allaah akupe umaizi na akuondoshee kizibo.

Hii ni nasaha yangu kwako. Pia ni nasaha kwa kila Salafiy anayekutakia kheri na kuchelea juu yako fikira zako hizi za ajabu na ufahamu wenye wenye kutia mashaka.

[1] 04:115

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 05/07/2020