Swali: Je, ni sahihi ya kwamba wataokunywa kwenye hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Ahl-us-Sunnah peke yake? Ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Dalili inapatikana kwenye maneno yetu [tuliyozungumza katika darsa]. Tumelizungumzia masaa. Tumesema kwamba hanywi kwenye hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa mwenye kushikamana na Sunnah zake. Kuhusiana na mtu wa Bid´ah na mwenye kuritadi hawatokunywa kwenye hodhi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_10.mp3
  • Imechapishwa: 26/06/2018