Ahl-us-Sunnah na Raafidhwah wana tofauti katika mataga peke yake?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema tofauti kati ya Ahl-us-Sunnah na Raafidhwah ni katika matawi peke yake?

Jibu: Hapana. Bali ni katika ´Aqiydah. Wanawaamini watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wana uwezo wa kudhuru na kunufaisha, wanawaomba pamoja na Allaah, wanawataka uokozi na wanawawekea nadhiri kama walivyokuwa wakifanya washirkina wa ki-Quraysh pamoja na al-Laat, al-´Uzzaa, Mitume na waja wema.

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayesema hivi?

Jibu: Huyu ni mjinga juu ya ´Aqiydah yao. Anatakiwa kubainishiwa na kuwekewa wazi ´Aqiydah yao. Hii ndio ´Aqiydah yao. Ni wenye kuchupa mipaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na khaswa al-Hasan, al-Husayn, Faatwimah na wasichana wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi yao khaswa kwa al-Hasan na al-Husayn. Wanafanya hivo kwa kuwa wanadai kuwa wananufaisha na wanawataka uokozi na wanawaomba wawaokoe kutokamana na adhabu ya Allaah. Baadhi yao vilevile wanaamini kuwa ´Aliy ndiye Mtume na kwamba Jibriyl alifanya khiyana juu ya utume na wanamwita kuwa ni “khaini”. Baadhi ya wengine wanachupa mipaka kwake na wanaitakidi kuwa ananufaisha pindi anapoombwa na anasaidia pindi anapotakwa uokozi. Kwa ajili hii wanaita “Ee ´Aliy”, “Ee al-Hasan”, “Ee al-Husayn”, “Ee Faatwimah” kama jinsi sisi tunavyoita “Ee Allaah”, “Ee Allaah”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 84
  • Imechapishwa: 07/12/2016