Ahl-ul-Kitaab wanapatikana leo?


Swali: Je, leo Ahl-ul-Kitaab wanapatikana na vipi tutawajua?

Jibu: Mayahudi na manaswara. Ahl-ul-Kitaab ni mayahudi na manaswara. Haya yanajulikana. Ni jambo linalojulikana manaswara hii leo wanawaita kuwa ni Masiyhiyyuun. Israaiyl wanawaita kuwa ni Yahuud. Hawa ndio Ahl-ul-Kitaab. Ni mayahudi na manaswara.

Mayahudi wao hawakubadili jina lao. Ama kuhusu manaswara wao wamebadili na kujiita “Masiyhiyyuun” badala ya manaswara pamoja na kwamba al-Masiyh (´Iysaa bin Maryam) yuko mbali na wao. Kujinasibisha naye sio sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (53) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-06-12.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014