Swali: Je, inajuzu kutukana dini iliyopotoshwa ambayo ni ya kiyahudi au kinaswara?

Jibu: Haitukanywi dini ambayo ina msingi na ina Mtume. Watu wake wanazo hukumu maalum ambapo wanaitwa “Ahl-ul-Kitaab”. Wataendelea kuitwa Ahl-ul-Kitaab mpaka kitaposimama Qiyaamah kwa ajili ya kuwapambanua na makafiri wengine ambao hawana Kitabu wala Mtume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 47
  • Imechapishwa: 04/06/2021