Ahl-ul-Bid´ah wao nyuma ya vyombo vya mawasiliano


Mfano wa hayo makundi mengine ni la kisiasa, ambalo linalingania watu kwenye maandamano. Na hiyo ni alama miongoni mwa alama za Khawaarij wa kale, wao na wanaowasaidia wote, na wanaopita katika njia yao au kuwanusuru kupitia intaneti, ni mamoja ikiwa ni iitwayo facebook au nyinginezo katika vifaa ambavyo vimekuwa ni sumu na makazi ya watu waasi na Ahl-ul-Bid´ah, vibaraka vya mayahudi na manaswara ambao wamefanya ufisadi katika miji mingi. Hakika kuwasaidia ni katika kusaidizana katika dhambi na uadui. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidianeni katika wema na uchaji Allaah wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Miongoni mwa hayo makundi maovu pia, ni yale makundi ambayo yanaona lengo nzuri linamjuzishia mtu njia. Wanaruhusu mambo ya haramu kwa ajili ya kufikia mambo yao maovu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=hptraXy0lTU
  • Imechapishwa: 06/09/2020