Swali: Baadhi wanakemea kutumia neon “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah” na wanaona kuwa badala yake mtu atumie neno “Salafiyyuun” au “Salaf”. Kwa sababu neno “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah” wanaingia ndani Ashaa´irah na Maaturiydiyyah.

Jibu: Ni kosa kuwaingiza Ahl-ul-Bid´ah, pasi na kujali Bid´ah zao, katika jina lisilofungamana na “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah”. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawaingii ndani yake wale watu wanaokwenda kinyume na Salaf katika ´Aqiydah na madhehebu yao. Kwa mfano ikiwa mtu huyu anapinga majina na sifa za Allaah basi sio katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika yale aliyopinga, ijapo anaweza kuingia katika wao katika mambo mengine. Kwa sababu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa mtu anaweza kukusanya kati ya Bid´ah na Sunnah, kufuru na imani. Tunasema mtu huyu ambaye ameenda kinyume na Salaf katika sifa za Allaah kwamba sio katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah inapokuja katika sifa za Allaah, ingawa anaweza kuwa ni katika wao katika mambo mengine kama mfano mambo ya Fiqh. Ni jambo lisilowezekana mzushi akawa ni miongoni mwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika ile Bid´ah yake. Hivyo tunaepuka utata huu ambao umepelekea kugongana kwa maoni ya wanachuoni.

Mimi naona kuwa Ahl-ul-Bid´ah sio katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika yale waliyozusha. Kwani Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawakuzusha Bid´ah hii. Ni vipi wanaweza kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ilihali wanaenda kinyume nao?

Swali: Je, msemo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah unatumika kwa Salafiyyuun?

Jibu: Hakuna haja ya hilo. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wale wenye kufuata yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa kundi lililookoka ni wale wenye kufuata yale aliyokuwa akifuata yeye na Maswahabah zake.

Swali: Kwa mfano tunasema kuwa an-Nawawiy na Ibn Hajar sio katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Ndio. Sio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika mtazamo wao wa majina na sifa za Allaah.

Swali: Tuseme kwa njia isiyofungamana kwamba sio katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Hatusemi kwa njia ya kuachia. Ndio maana nimesema kuwa yule anayekwenda kinyume na Salaf katika sifa za Allaah haitwi moja kwa moja kwamba ni “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah”. Bali inatakiwa kusema kwa njia iliyofungamana na kusema kwamba ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa mfano katika Fiqh, lakini sio katika mambo ya Bid´ah zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (8 B)
  • Imechapishwa: 31/05/2020