Swali: Wakati Allaah (Ta´ala) aliposema:

وَيَبْقَى وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَامِ

“Utabaki Uso wa Mola wako, wenye utukufu na ukarimu.” (55:27)

Ni sawa kusema kwamba uso ni dhati ya Allaah?

Jibu: Ndio. Aayah inathibitisha uso na dhati vyote viwili. Lakini Ahl-ul-Bid´ah wanafasiri kuwa ni dhati pekee ndio itabaki na wanapinga uso. Aayah inamthibitishia uso Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 17/03/2019