Ahl-ul-Bid´ah ndio wanaojibidisha na ´ibaadah katika Rajab


Swali: Nimenuia kufanya ´Umrah katika wiki hii. Lakini hata hivyo kuna baadhi ya watu wamenishauri niiache na badala yake niifanye katika mwezi mwigine ili nisije kujifananisha na Ahl-ul-Bid´ah ambao wanafanya ´Umrah tarehe 27 katika mwezi huu wa Rajab.

Jibu: Ndio, ni kweli. Icheleweshe ´Umrah mpaka utakapokwisha utata huu. Kwa sababu wale wazushi ndio wanaofanya ´Umrah katika Rajab. Kwa hivyo jiepushe na hilo ili usishirikiane ijapokuwa hukuwa ni mwenye kukusudia hilo. Lakini hata hivyo ndani yake kuna kushirikiana nao na kujifananisha nao. Icheleweshe ´Umrah wakati mwingine mbali na Rajab.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/3512
  • Imechapishwa: 31/03/2018