Afupishe swalah katika yale masiku mane ya mwanzo?


Swali: Mtu akinuia kubaki sehemu zaidi ya siku nne afupishe katika zile siku nne za mwanzo kisha aanze kuswali kikamilifu kuanzie ile siku ya tano?

Jibu: Hapana. Tokea siku ya kwanza aliyofika asifupishe midhali amenuia kubaki sehemu hiyo zaidi ya siku nne. Anatakiwa kuswali kikamilifu tokea siku ile aliyofika katika mji aliyonuia kubaki ndani yake zaidi ya siku nne.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017