Afanye Tayammum na kuswali ndani ya wakati au aoge ijapo ataswali baada ya wakati kumalizika?

Swali: Mara inatokea naamka kutoka usingizini nikiwa na janaba. Je, ni lazima kwangu kufanya Tayammum na kuswali ndani ya wakati pamoja na wengine au nioge hata kama utatoka nje ya wakati wa swalah?

Jibu: Ni lazima kwako kuoga unapotaka kuswali. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi…”

mpaka aliposema:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni.”[1]

Kwa hivo ni lazima kuoga ijapo utatoka nje wakati wa swalah kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru. Kujitwahirisha kutokamana na hadathi ni sharti ya kusihi kwa swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hakubali swalah ya mmoja wenu anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

[1] 05:06

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (04/145) nr. (16577 )
  • Imechapishwa: 05/06/2022