Afanye nini mzee asiyeweza kufunga?

Swali: Sisi tuko na mama mtumzima na hawezi kufunga. Afanye nini?

Jibu: Analazimika kuwalisha masikini kwa kila siku moja karibu 1,5 kg ya chakula kinacholiwa katika mji katika tende, mchele au vyengine. Hivyo ndivyo walivyojibu kundi katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Miongoni mwao ni Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhum). Akiwa ni fakiri asiyeweza kulisha basi hakuna kinachomlazimu. Kafara hii inafaa kwake kuitoa kwa wakati mmoja au nyakati mbalimbali. Ni mamoja mwanzoni mwa mwezi, katikati ya mwezi au mwishoni mwa mwezi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/274)
  • Imechapishwa: 08/06/2018